Tuesday, May 1, 2012

Wizara ya Uchukuzi siku ya Ijumaa tarehe 27 Aprili 2012 ilizindua rasmi Baraza lake la Wafanyakazi. Uzinduzi wake ulifanyika Mkoani Tanga katika Hoteli ya Mkonge na Waziri wa Uchukuzi Mhe Omari R. Nundu(Mb).



Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi Bibi J. Ndaba, Bw. E. Mkiaru(mwenye suti nyeusi), Bw L. Lwiza (mwenye tai nyeusi) na Bibi J. Akile (aliyevaa kitenge) wakijadiliana jambo wakati wakisubiri ujio wa Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye ni Katibu Mkuu Mhandisi Omar A. Chambo.


Mjumbe Bw. T. Kasambala(mwenye shati jekundu) akibadilishana mawazo na na mjumbe mwenzie Bw. B.Chiganga(aliyesimama)kabla ya kuwasili kwa Mwenyekiti wa Baraza Mhandisi Omar A. Chambo.


Wajumbe wa Baraza Bi. A. Selemani(mwenye ushungi) na Bw. Ndumbaro(mwenye suti nyeusi) wakiteta jambo kabla ya kuanza kikao cha Baraza.


Wajumbe wakipitia vitabu vyenye taarifa za kikao kabla ya uzinduzi wa Baraza.



Wajumbe Bw. E. Mgawe(wa kwanza kushoto), Bw Manongi(wa pili kushoto), Bw N. Kirenga(wa pili toka kulia) na Dkt. ...(wa kwanza kulia)wakibadilishana mawazo kabla ya uzinduzi wa Baraza.








Wajumbe wakibadilishana mawazo na kupitia makabrasha kabla ya kuanza kwa kikao cha baraza.




Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu(DAHRM) Bibi J. Ndaba akimkaribisha Mwenyekiti wa Baraza Mhandisi Omar A. Chambo(aliyekaa katikati) kabla ya kufungua kikao cha baraza. Kushoto kwa Mwenyekiti katika picha ni Bw.Matiku - Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi(TUGHE) Wizarani, Mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi Mkoa(mwenye kofia) na Mwezeshaji toka Wizara ya Kazi na Ajira(mwenye suti ya kijivu).


Kamati ya Uchaguzi ikihesabu kura za majina yaliyopendekezwa kuongoza baraza yaani Katibu na Naibu Katibu ambapo Bw. Hassan Mabula alichaguliwa kuwa Katibu na Bibi Ruth Kigera alichaguliwa kuwa Naibu Katibu.


Mwenyekiti wa Baraza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo(wa kwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi  wa Huduma za Uchukuzi Mhandisi Saad Fungafunga(katikati) na Katibu wa Baraza Bw. Hassan Mabula(kushoto) wakimsubiri Waziri wa Uchukuzi Mhe. Omari R. Nundu kabla ya uzinduzi wa Baraza.



Mwenyekiti wa Baraza Mhandisi Omar A. Chambo pamoja na Wakuu wa Taasisi na Idara/Vitengo wakimsubiri Waziri wa Uchukuzi Mhe.Omari R. Nundu.


Waziri wa Uchukuzi Mhe. Omari R. Nundu(Mb) akisalimiana/akipokewa na Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi Mhandisi S. Fungafunga kabla uzinduzi wa Baraza. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Baraza Mhandisi Omar A. Chambo pamoja na Wakuu wa Idara na Taasisi zilizo chini ya Wizara.



Waziri wa Uchukuzi Mhe. Omari R. Nundu akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Baraza Mhandisi Omar A. Chambo pamoja na Wakuu wa Idara na Taasisi zilizo chini ya Wizara kabla ya kuzindua Baraza.










Waziri wa Uchukuzi Mhe. Omari R. Nundu akisalimiana na Wakuu wa Taasisi na Idara wakati akiingia katika Ukumbi wa Mkutano wa Hoteli ya Mkonge kuzindua Baraza.


Baadhi ya wajumbe wa Baraza(kutoka kushoto) Bw Butallah, Bw. Chande na Bw. Mangosongo wakimkaribisha ukumbini Waziri wa Uchukuzi Mhe. Omari R. Nundu(hayupo pichani).




Saturday, March 17, 2012


KONGAMANO LA KITAIFA LA USAFIRI WA ANGA (NATIONAL AIR TRANSPORT FORUM) TAREHE 21-22 MACHI 2012





Wizara ya Uchukuzi kwa kushirikiana na Sekta binafsi imeandaa Kongamano la Taifa la Usafiri wa Anga litakalofanyika Dar es Salaam kwenye Hoteli ya Serena zamani Movenpick kuanzia tarehe 21 - 22 Machi, 2012.

Kongamano hili litajadili maendeleo ya Usafiri wa Anga hapa nchini, changamoto zinazokabili sekta ya anga na namna ya kubaliana nazo. Aidha,  washiriki pia watajadili kwa kina mchango unaoweza kutolewa na usafiri wa Anga katika  ukuaji wa pato la Taifa.

Washiriki wa Kongamano hili ni wadau kutoka sekta ya usafiri wa anga wa ndani na nje ya nchi pamoja na sekta nyingine kama vile Fedha, Nishati na Madini, Mawasiliano, Uchukuzi, hali ya Hewa na nyinginezo.

Kongamamo hilo litaanza saa 3.00 asubuhi

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ifuatayo: http://www.newhorizonstz.com

Wednesday, January 4, 2012

Taarifa kwa Umma na Vyombo vya Habari kuhusu urudishwaji wa huduma ya Usafiri wa Reli ya Kati

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) una furaha kuwataarifu kuwa kuanzia leo Januari 04, 2012 imerejesha huduma zake katika reli ya kati . Ambapo treni 4 za mizigo zimepangwa kuanzia safari kutokea Mororgoro kwenda Tabora, 2 kati ya hizo zimeshaondoka Morogoro kati ya saa 7 na 9 usiku kuamkia leo wakati nyingine 2 zilitarajiwa kuondoka saa 2 na 5 asubuhi leo.
Wakati huo huo huduma ya usafiri wa treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma imepangwa kuanza tena hapo siku ya Jumamosi Januari 07, 2012 saa 11 jioni, na kwamba wananchi wote ambao wanapendelea kusafiri na treni hiyo wafike katika stesheni zilizokaribu yao kukata tiketi za safari kuanzia leo Jumatano Januari 04, 2012.

Uamuzi wa kuanza kutoa huduma unatokana na kukamilika kwa matengenezo ya reli katika maeneo mbalimbali ya reli ya kati kuanzia mkoani Dar es Salaam, Pwani na Dodoma na hasa maeneo ya Gulwe na Godegode mkoani Dodoma ambayo yaliathirika sana na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa na Dodoma.

Wahandisi na mafundi wa TRL walikuwa wanafanya kazi za ukarabati maeneo husika saa 24 bila ya kujali mapumziko na hivyo kuwezesha kukamilika kwa kazi za ukarabati kwa wakati. Aidha ziara za viongozi wa ngazi za juu wa Wizara ya Uchukuzi akiwemo Waziri, Mhandisi Omari R. Nundu na Katibu Mkuu Mhandisi Omar A. Chambo ziliwapa motisha wa kukamilisha kazi ya ukarabati kwa wakati.

Huduma za usafiri na usafirishaji zilisimamishwa rasmi katika reli ya kati kuanzia Desemba 20 mwaka jana ambapo Uongozi wa TRL ulilazimika kukodi mabasi yapatayo 25 siku ya Desemba 21, 2011 kuwasafirisha abiria 1834 wa treni waliokuwa wamekwama Dodoma wakitokea Kigoma kutokana na eneo la reli ya kati ya Stesheni za Gulwe na Godegode mkoani Dodoma tuta lake kusombwa na mafuriko ya mvua zinazoendelea nchini.

Taarifa hii imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Mhandisi K.A.M.Kisamfu.


MIDLADJY MAEZ
MENEJA UHUSIANO - TRL
DAR ES SALAAM.
JANUARI 04, 2012



Tuesday, December 27, 2011

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU RELI YA KATI
Kutokana na Mvua kubwa zinazonyesha maeneo mbalimbali ya reli ya Kati, Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umeamua kuchukua uamuzi wa kufuta safari zote za Treni za abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kuanzia leo Jumanne Desemba 27, 2011 hadi itakavyotangazwa vinginevyo.

Kwa hiyo basi abiria wote waliokuwa wamepanga kusafiri leo na pia katika treni zijazo wanatakiwa kufika na tiketi zao katika ofisi za Stesheni Masta husika ili warejeshewe fedha za nauli walizolipa.

Tafadhali atakayesoma habari hii awaarifu na wengine.

Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu wote uliojitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano -TRL


TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa hii inatoa mwelekeo wa mabadiliko ya mifumo ya hali ya hewa na mvua kuanzia mwezi Desemba 27, 2011 kuelekea mwaka mpya 2012. Ukanda wa mvua unatarajiwa kuimarika maeneo mengi nchini na mvua zinatarajiwa kuanza kwenye ukanda wa pwani kesho ukiwemo mkoa wa Dar es salaam na kuongezeka kuelekea mwaka mpya 2012.

Mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuimarika kwa hali ya joto la Bahari ya Hindi, sambamba na kuongezeka kwa msukumo wa hewa yenye unyevunyevu kutoka misitu ya Kongo na kusababisha makutano ya upepo katika eneo la mashariki na kusini magharibi mwa nchi kuanzia Disemba 28, 2011 kuelekea mwaka mpya 2012. Hali hii inatarajiwa kusababisha kuanza kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi hapa nchini.

Maeneo ya mikoa ya ukanda wa pwan(mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi na Kisiwa cha Unguja), Nyanda za juu kusini magharibi(Mikoa ya Mbeya, Iringa na Rukwa), kanda ya kati(Mikoa ya Dodoma na Singida) na magharibi mwa nchi(Mikoa ya Kigoma na Tabora) na maeneo machache ya Nyanda za juu kaskazini Mashariki(mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara) yanatarajiwa kuwa na  vipindi vya mvua kubwa.

Kufuatia viwango vikubwa vya mvua vilivyonyesha, ongezeko kidogo la mvua linatarajiwa kusababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu. Mamlaka inashauri tahadhari stahiki ziendelee kuzingatiwa.

Maeneo mengine ya nchi yanatarajiwa kupata mvua za kawaida katika kipindi hicho.

Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya Hali ya hewa na athari zake na itaendelea kutoa taarifa na tahadhari kila inapobidi.


  
 Dkt. Agnes Kijazi
 Mkurugenzi Mkuu  
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Saturday, December 3, 2011

Rais wa Zanzibar afungua Rasmi maonesho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara - Viwanja vya JK Nyerere (Viwanja vya Sabasaba)


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na viongozi wengine wa Serikali pamoja na wananchi na wadau mbalimbali wakisubiri ujio wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo akiteta jambo wakati wakisubiri ujio wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Ali Mohamed Shein.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein (wa tatu kutoka kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji Dk Mary Nagu (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo (wa kwanza kulia), viongozi wengine wa Serikali na wadau mbalimbali wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya Rais kuwasili.




 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo (wa pili toka kulia) pamoja voingozi wengine wa Serikali wakiangalia ngoma za asili wakati wa ufunguzi wa maonesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.


Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho na Sherehe za Taifa Philemon Luhanjo akiwakaribisha Mgeni wa Heshima, viongozi wa Serikali na wageni wengine waalikwa.


Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wakisikiliza hotuba ya ukaribisho ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho na Sherehe za Taifa Philemon Luhanjo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji Dk Mary Nagu akielezea manufaa ya maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara huku Mgeni Rasmi na viongozi wengine wa Serikali wakimsikiliza.

Mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Ali Mohamed Shein akihutubia viongozi wa serikali, wageni waalikwa, wananchi na wadau mbalimbali waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa maonesho. Wengine katika picha wakimsikiliza mgeni rasmi ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji Dk Mary Nagu(mwenye kofia nyekundu).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi atembelea Banda la Sekta ya Uchukuzi katika Viwanja vya JK Nyerere


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo (wa kwanza kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhandisi Mussa Iyombe (wa kwanza kushoto) na viongozi wengine wa Serikali wakitoka katika Ukumbi wa Rashid Kawawa baada ya uzinduzi rasmi wa maonesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo  akikaribishwa na "Air Hostess" wa Kampuni ya Ndege ya Tanzania katika Banda la Wizara ya Uchukuzi na Taasisi zilizo chini yake ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo akisaini kitabu cha Wageni katika Banda la Wizara ya Uchukuzi huku watumishi wa Wizara Ndg. Lwiza na Bi. Sanda wakishuhudia.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo akipata maelezo ya nini kinafanyika katika Wizara yake toka kwa Bi. Sanda ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo akisaini kitabu cha wageni katika banda la Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO) huku watumishi wake Bi. Amina Good, Bw. Michael Semaya na Bw. Bryson Munuo wakishuhudia.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo akidadisi jambo toka kwa watumishi wa kampuni ya RAHCO.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo akisaini kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Reli la Tanzania (TRL) huku watumishi wake.