Tuesday, December 27, 2011

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU RELI YA KATI
Kutokana na Mvua kubwa zinazonyesha maeneo mbalimbali ya reli ya Kati, Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umeamua kuchukua uamuzi wa kufuta safari zote za Treni za abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kuanzia leo Jumanne Desemba 27, 2011 hadi itakavyotangazwa vinginevyo.

Kwa hiyo basi abiria wote waliokuwa wamepanga kusafiri leo na pia katika treni zijazo wanatakiwa kufika na tiketi zao katika ofisi za Stesheni Masta husika ili warejeshewe fedha za nauli walizolipa.

Tafadhali atakayesoma habari hii awaarifu na wengine.

Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu wote uliojitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano -TRL


TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa hii inatoa mwelekeo wa mabadiliko ya mifumo ya hali ya hewa na mvua kuanzia mwezi Desemba 27, 2011 kuelekea mwaka mpya 2012. Ukanda wa mvua unatarajiwa kuimarika maeneo mengi nchini na mvua zinatarajiwa kuanza kwenye ukanda wa pwani kesho ukiwemo mkoa wa Dar es salaam na kuongezeka kuelekea mwaka mpya 2012.

Mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuimarika kwa hali ya joto la Bahari ya Hindi, sambamba na kuongezeka kwa msukumo wa hewa yenye unyevunyevu kutoka misitu ya Kongo na kusababisha makutano ya upepo katika eneo la mashariki na kusini magharibi mwa nchi kuanzia Disemba 28, 2011 kuelekea mwaka mpya 2012. Hali hii inatarajiwa kusababisha kuanza kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi hapa nchini.

Maeneo ya mikoa ya ukanda wa pwan(mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi na Kisiwa cha Unguja), Nyanda za juu kusini magharibi(Mikoa ya Mbeya, Iringa na Rukwa), kanda ya kati(Mikoa ya Dodoma na Singida) na magharibi mwa nchi(Mikoa ya Kigoma na Tabora) na maeneo machache ya Nyanda za juu kaskazini Mashariki(mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara) yanatarajiwa kuwa na  vipindi vya mvua kubwa.

Kufuatia viwango vikubwa vya mvua vilivyonyesha, ongezeko kidogo la mvua linatarajiwa kusababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu. Mamlaka inashauri tahadhari stahiki ziendelee kuzingatiwa.

Maeneo mengine ya nchi yanatarajiwa kupata mvua za kawaida katika kipindi hicho.

Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya Hali ya hewa na athari zake na itaendelea kutoa taarifa na tahadhari kila inapobidi.


  
 Dkt. Agnes Kijazi
 Mkurugenzi Mkuu  
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Saturday, December 3, 2011

Rais wa Zanzibar afungua Rasmi maonesho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara - Viwanja vya JK Nyerere (Viwanja vya Sabasaba)


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na viongozi wengine wa Serikali pamoja na wananchi na wadau mbalimbali wakisubiri ujio wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo akiteta jambo wakati wakisubiri ujio wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Ali Mohamed Shein.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein (wa tatu kutoka kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji Dk Mary Nagu (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo (wa kwanza kulia), viongozi wengine wa Serikali na wadau mbalimbali wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya Rais kuwasili.




 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo (wa pili toka kulia) pamoja voingozi wengine wa Serikali wakiangalia ngoma za asili wakati wa ufunguzi wa maonesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.


Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho na Sherehe za Taifa Philemon Luhanjo akiwakaribisha Mgeni wa Heshima, viongozi wa Serikali na wageni wengine waalikwa.


Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wakisikiliza hotuba ya ukaribisho ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho na Sherehe za Taifa Philemon Luhanjo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji Dk Mary Nagu akielezea manufaa ya maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara huku Mgeni Rasmi na viongozi wengine wa Serikali wakimsikiliza.

Mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Ali Mohamed Shein akihutubia viongozi wa serikali, wageni waalikwa, wananchi na wadau mbalimbali waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa maonesho. Wengine katika picha wakimsikiliza mgeni rasmi ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji Dk Mary Nagu(mwenye kofia nyekundu).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi atembelea Banda la Sekta ya Uchukuzi katika Viwanja vya JK Nyerere


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo (wa kwanza kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhandisi Mussa Iyombe (wa kwanza kushoto) na viongozi wengine wa Serikali wakitoka katika Ukumbi wa Rashid Kawawa baada ya uzinduzi rasmi wa maonesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo  akikaribishwa na "Air Hostess" wa Kampuni ya Ndege ya Tanzania katika Banda la Wizara ya Uchukuzi na Taasisi zilizo chini yake ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo akisaini kitabu cha Wageni katika Banda la Wizara ya Uchukuzi huku watumishi wa Wizara Ndg. Lwiza na Bi. Sanda wakishuhudia.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo akipata maelezo ya nini kinafanyika katika Wizara yake toka kwa Bi. Sanda ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo akisaini kitabu cha wageni katika banda la Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO) huku watumishi wake Bi. Amina Good, Bw. Michael Semaya na Bw. Bryson Munuo wakishuhudia.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo akidadisi jambo toka kwa watumishi wa kampuni ya RAHCO.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo akisaini kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Reli la Tanzania (TRL) huku watumishi wake.

Friday, December 2, 2011

Wizara ya Uchukuzi na Taasisi zake waanza wiki ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru katika Viwanja vya SabaSaba Kilwa Road kuanzia 1-9 Desemba 2011




Karibu sana katika Banda la Sekta ya Uchukuzi ambalo lipo katika Jengo la VETA ambapo utakaribishwa na wadada watanashati, warembo, wenye bashasha na wakarimu.


Watumishi wa Wizara Bw. Mkiaru na Bi. Sanda wakipeana mawazo ya  maandalizi ya mwisho ya banda lao.


Baada ya maandalizi, watumishi wa Wizara Bw. Biseko na Bw. Mashaka wakitafakari mpangilio mzima.