Friday, September 16, 2011

Naibu Waziri wa Uchukuzi aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa eneo la kutunzia Makasha katika Bandari ya Dar es Salaam


Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Athumani R. Mfutakamba,akiweka jiwe la msingi la eneo la kutunzia makontena Katika Bandari ya Dar es Salaam. Tukio hilo lilifanyika ikiwa ni sehemu maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Sekta ya Uchukuzi.Kushoto kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar A. Chambo na wa pili kulia kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Ndg. Ephraim Mgawe na viongozi wengine wa Wizara na Taasisi zilizochini ya Wizara ambao walikuwepo kushuhudia tukio hili muhimu.

Naibu Waziri wa Uchukuzi afungua kongamano la Usafirishaji


Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Athumani R. Mfutakamba akifungua Kongamano la Usafirishaji lilloandaliwa na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)  katika hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza. Lengo la Kongamano hili lilikuwa kujadili maendeleo, changamoto na matarajio ya Sekta ya Usafirishaji  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Thursday, September 15, 2011

Mikataba ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege vya Bukoba, Kigoma na Tabora




Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA), wawakilishi toka Kampuni ya Ujenzi ya China na Wageni waalikwa wakimsubiri Mgeni wa Heshima, Waziri wa Uchukuzi Mhe Omari R. Nundu(MB) na Viongozi wengine wa Wizara na Kampuni itakayojenga Viwanja vya Ndege vya Bukoba, Tabora na Kigoma.


Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Omari R. Nundu (Mb) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar A. Chambo kabla ya tukio la utiaji saini mikataba ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege vya Bukoba, Tabora na Kigoma kwa kiwango cha Lami. Kulia kwa Katibu Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Ndg. John T. Mngodo.


Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi ya Utiaji saini Mikataba ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege vya Bukoba, Tabora na Kigoma iliyokuwa ikisomwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Mhandisi Suleiman S. Suleiman (Hayupo Pichani).


Mgeni Rasmi waziri wa Uchukuzi, Mhe. Omari R. Nundu akiongea na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA), Wawakilishi wa kampuni ya ujenzi ya China, Viongozi wa Wizara na Taasisi pamoja na wadau mbalimabli waliohudhuria tukio la Utiaji saini Mikataba ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege vya Bukoba, Tabora na Kigoma. Kushoto kwa Waziri ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Athumani R. Mfutakamba.


Wawakilishi toka Kampuni ya Ujenzi ya China wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Omari R. Nundu ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika tukio la Utiaji saini wa Mikataba ya Ujenzi ya Viwanja vya Ndege vya Bukoba, Tabora na Kigoma.





Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar A. Chambo(Wa tatu toka kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Ndg. John T. Mngodo(wa pili toka kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Waziri wa Uchukuzi Mhe. Omari R. Nundu.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) Mhandisi Suleiman S. Suleiman na Mwakilishi wa kampuni ya Ujenzi ya China wakisaini Mikataba ya ujenzi wa viwanja vya ndege vya Bukoba, Tabora na Kigoma. (Mstari wa Nyuma)Wakishuhudua tukio hilo ni Waziri wa Uchukuzi Mhe.Omari R. Nundu (wa pili toka kushoto), Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Athumani R. Mfutakamba(wa tatu kutoka kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo(wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Ndg. John T. Mngodo(wa tatu toka kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi Mhandisi Majura (wa kwanza kushoto) na viongozi wengine wa Wizara na wawakilishi wa kampuni ya China.

Waziri wa Uchukuzi,Mhe. Omari R. Nundu(katikati), Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.Dkt. Athumani R. Mfutakamba(wa tatu kutoka kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar A. Chambo(wa tatu kutoka kulia),Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Ndg. John N. Mngodo (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Mhandisi. Suleiman S. Suleiman (wa pili kutoka kushoto) na wawakilishi toka Kampuni ya Ujenzi ya China katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Wakurugenzi wa Wizara na Taasisi mbalimbali zilizochini ya Wizara baada ya kusaini Mikataba ya ujenzi wa viwanja vya Bukoba, Tabora na Kigoma. Tukio hilo lilifanyika katika maeneo ya Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA), Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar A. Chambo(wa pili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) Mhandisi Suleiman S. Suleiman (wa pili kutoka kulia) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kampuni ya Ujenzi ya China baada ya tukio la utiaji saini Mikataba ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege vya Bukoba, Tabora na Kigoma.